Happy Birth Day Kkkt Dayosisi Ya Mwanga

By EM123456 September 6, 2016 40 views 0 comments

"˜"˜HAPPY BIRTH DAY KKKT DAYOSISI YA MWANGA''

Hatimaye Dayosisi ya Mwanga ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), imezaliwa baada ya kuchukua miaka 18 tangu vuguvugu la kuanzishwa kwake lilipoanza

Kwa ufupi Mkutano mkuu wa kuzaliwa kwa dayosisi hiyo umehudhuriwa na Mkuu wa Kanisa hilo, Askofu Dk Fredrick Shoo, Waziri mkuu mstaafu, Cleopa David Msuya na maaskofu
Daniel Mjema

Mwanga. Hatimaye Dayosisi ya Mwanga ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), imezaliwa baada ya kuchukua miaka 18 tangu vuguvugu la kuanzishwa kwake lilipoanza.

Mkutano mkuu wa kuzaliwa kwa dayosisi hiyo umehudhuriwa na Mkuu wa Kanisa hilo, Askofu Dk Fredrick Shoo, Waziri mkuu mstaafu, Cleopa David Msuya na maaskofu.

Dayosisi hiyo ambayo imezaliwa kutoka Dayosisi ya Pare inayoongozwa na Askofu Charles Mjema, inafanya idadi ya Dayosisi za KKKT nchini kufikia 25.

Katika mkutano huo, Mchungaji Chediel Sendoro amechaguliwa kuwa Askofu Mteule.

Askofu Shoo amesema Mchungaji Sendoro amechaguliwa kushika wadhifa huo baada ya kupata kura 62 kati ya kura 77 zilizopigwa wa wajumbe.

Pia, wamemchagua Mchungaji Timoth Msangi kuwa Msaidizi wa Askofu Mteule baada ya kupata kura 78 huku kura tano zikimkataa.

Askofu Shoo amesema viongozi hao wataendelea kuwa wateule hadi watakapowekwa wakfu na kuingizwa kazini.

Askofu wa Dayosisi ya Pare ambayo ndiyo iliyozaa Dayosisi ya Mwanga, Mjema, amesema tukio hilo ni la kihistoria na linahitimisha safari ya miaka 18

"Itakuwa ni hatua ya kuhitimisha safari yetu ya miaka 18 iliyokuwa imejaa changamoto nyingi na kutupa uzoefu wa aina yake katika kuhudumiwa Kanisa la Mungu.

"Hakuna aliyeshinda au kushindwa wala hakuna aliyefanya zaidi ya mwingine kwa kila mmoja kwa nafasi yake alifanya kilichokuwa wajibu wake," amesema Askofu Mjema.

Related Surnames:
ELIASMARTINMRUTU

No comments yet.