Tawala Za Kiimla Duniani Na Sifa Zake

By EM123456 September 6, 2016 43 views 0 comments

TAWALA ZA KIIMLA DUNIANI NA SIFA ZAKE
By Mrutu E.M
Udikteta ni hali ya kuwa na utawala ambao haufuati misingi ya kidemokrasia kwa wananchi wake wanaowaongoza.
Utawala huo hutoa maelekezo na kutaka yafuate kama yalivyo bila kuhoji wala kuuliza.
Viongozi hao hupatikana kwa njia kuu tatu ambazo ni.

1. Kupindua serikali iliyopo madarakani na kujipachika madaraka makubwa sana na kusitisha katiba na vyama vya siasa.
2. Kuchaguliwa na wananchi na kubadili katiba na kuongeza kwa mabavu bila kufuata katiba.
3. Kurithi utawala kutoka kwa wazazi, ndugu, jamaa na marafiki.
Mfano wa madikteta duniani ni kama ifuatavyo.
1. Zaire(1960-1997) Mobutu Seseseko Ngbendu kuku wa Zebanga.
2. Afrika ya kati Bokasa.
3. Nigeria (1991-1996) Jenerali Sani Abacha.
4. Guinea Jenerali Robert Guiey
5. Sudani(1980 hadi sasa) Jenerali Omary Hassan El bashir.
6. Uganda (1971-1979) Jen. Idd Amin Dadaa.
7. Yugoslavia hadi 1997 Slobodan Milosevic.
Hao ni baadhi tu ya madikteta waliokuwepo duniani.

SIFA ZA MADIKTETA (5P)
Madikteta au watawala wa kiimla wana sifa kuu tano ambazo zinafanana kwa wote. Hata hivyo hutofautiana kutegemeana na mahali na wakati husika wa utawala. Pia hutofautiana kulingana na namna walivyoingia.

SIFA AU TABIA HIZO
Sifa hizo au 5p ni (Property, Power, Prestige, Popularity, Pomposity)
1. PROPERTY.
Viongozi wa aina hiyo hupenda Mali kuliko utu, huweza kuwafukuza watu kazi, kuwafunga, kutaifisha mali na kuwauwa watu wake kwa sababu anataka kulimbikiza Mali au kukusanya mapato hata kama ni kwa njia haramu.
Kumbuka katika soko huria kila kitu kinaweza kuuzika na kununulika hata kama ni mtu au Mali zake au utu wake.
2. POWER.
To be a victim of power. Ni kiongozi ambaye hupenda kuwa na madaraka makubwa sana na mwenye nguvu sana za kiutawala.
3. PRESTIGE.
Hii ni hali ya kupenda kuheshimiwa hata kama hana sifa wala mambo ya maana anayoyafanya katika uongozi wake. Mfano ni wabunge wa Tanzania ambao wiki iliyopita walihoji kwa waziri wa mambo ya ndani kupitia kipindi cha maswali bungeni kwamba kwanini askari wa majeshi mbalimbali hawawapigii saluti? Ni hatua gani askari wanachukuliwa kwa kutowapigia saluti?.
Mfano mwingine ni aliyekuwa Rais wa Kenya 1978-2002 Daniel Toroitch Arap Moi ambaye alipenda kuitwa mtukufu Rais badala ya ndugu au mheshimiwa.
4. POPULARITY.
Hii ni kitendo cha kutaka umaarufu kwa njia yoyote. Umaarufu huo hujengwa kwa kutumia nguvu na vyombo vya dola na kuitungia jamii sheria kila siku za kuendelea kuwabana na kuwakandamiza.
5. POMPOSITY.
Prosperity ni kupenda mbwembwe bila sababu. Hupenda kuwa na misafara mikubwa sana bila msingi wowote. Ni waoga sana kuhujumiwa hivyo huwa na ulinzi mkali sana na wa gharama za hali ya juu sana. Mfano ni alivyokuwa Kanal Muhamar Ghadafi ambaye msafara wake ulikuwa wa magari 60 na helicopter moja na walinzi 300 kwa msafara mmoja. Hupenda kusifiwa sana na kutukuzwa. Uchaguzi hufanyika tu ili kuonekana kwamba palifanyika uchaguzi lakini uhesabuji na utangazaji wa matokeo ni siri ya watawala hao.
NB; Ifahamike kwamba.
1. Nigeria imeshuhudia mapinduzi ya kijeshi Mara 9 tangu Uhuru mwaka 1960. Miongoni mwa viongozi wa kijeshi waliopita Nigeria ni.
1. Jenerali Olusegan Ezekiel Ongindo Obasanjo 1975-1977 na kuchagul kwa kura 1996-2006.
2. Mahamoud Bohari 1980-1983 pia alichaguliwa kuwa Rais 2015 hadi sasa baada ya kumshinda Rais Goodluck Jonathan aliyeshika madaraka baada ya kifo cha Rais Umaru Musa Yar adua.
3.Ibrahim Babangida Hadi 1991
4. Jenerali Sani Abacha 1991-1996 na alifariki akiwa akiwa madarakani wakati akijiandaa kuvua gwanda na kavaa suti.
5. Jenerali Atik Abubakary 1996-1996 ambaye aliteuliwa na jeshi kufuatia kifo cha Jenerali Sani Abacha. Hata hivyo aligoma kusalia madarakani na kuitisha uchaguzi na kukabidhi utawala wa kiraia kwa Jenerali Olusegun Obasanjo mwaka 1996
Obsanjo amekuwa rais wa kwanza wa Nigeria wa kuchaguliwa na kumaliza muhula wake na kukabidhi utawala mwingine wa kidemokrasia tangu uhuru mwaka 1960.
Visiwa vya Comoro navyo vimeshuhudia mapinduzi mara 27 tangu vijinyakulie uhuru wake kutoka kwa ufaransa ambavyo makao makuu yake ni moroni katika kisiwa cha ngazija. Commoro inaundwa na visiwa vikuu vine ambavyo ni Ngazija, Mayote, Muheli na Anjuani ambavyo Ufaransa inashikilia kisiwa cha Mayote hadi sasa.
Hadi kufikia miaka ya 1990 bara la afrika bado lilikuwa linakumbwa sana na mapinduzi ya kijeshi ila kuanzia miaka ya 2000 hali hiyo imepungua kwa kiwango kikubwa sana. Hadi ya udikteta uliobaki ni wa kuchaguliwa na kurithi.
Kuna viongozi wengi ambao baada ya kuingia kupitia mapinduzi ya kijeshi baadae walichaguliwa na kuendelea kusalia mamlakani kwa kipindi kirefu sana wakidai kwamba bado wanapendwa na wananchi wao. Viongozi hao huitisha chaguzi mara kwa mara lakini huwaamulia tume za uchaguzi aina ya matokeo wanayoyataka. Wengine waliingia kupitia uchaguzi lakini baadae hunogewa na madaraka na kugoma kuondoka madarakani hata kama kunatokea umwagikaji wa damu, mfano ni Rais wa Burundi Piere Nkurunziza ambaye aliamua kugombea muhula wa tatu kinyume na katiba na kusababisha umwagikaji wa damu na kupelekea wakimbizi wengi kukimbilia Tanzania.
Viongozi wengi huingia kwa kurithi ama kujipachika madaraka baada ya wazazi wao kufariki, mfano ni Rais wa DRC Joseph Kabila Kabange ambaye aliingia madarakani baada ya kifo cha Rais Laurent desire kabila ambaye alikuwa baba yake. Rais Ally ben bongo wa gabon ambaye aliingia madarakani kufuatia kifo cha baba yake omary bongo ambaye alikaa madarakani kwa zaidi ya miaka 30. Fohre Gnasimbe wa mali ambaye aliingia madarakani kufuatia kifo cha baba yake Gnasimbe Eyadema ambaye alikaa madarakani kwa muda mrefu hadi kifo chake. Ikumbukwe kwamba nchi hizo hazina utawala wa kifalme ili waweze kurithi uongozi kifamilia.

NINI KIFANYIKE
1. Umoja wa Afrika na taasisi mbalimbali duniani ziendelee kuhimiza utawala wa kidemokrasia kama walivyoweza kukomesha mapinduzi ya kijeshi afrika.
2. Viongozi wanaosababisha matatizo hayo kwa watu wake washitakiwe ili kuwe na fundisho kwa wengine wenye uchu kama wao.
3. Katiba za nchi husika zirekebishwe ama ziandikwe upya ili kuweza kuwawajibisha watu wa aina hiyo.
4. Kuondolewe mfumo wa kaifalme ili kupanua wigo wa demokrasia duniani.
5. Kuwepo na mfumo sawa kwa mataifa yote ya kaifrika ya mihula ya uongozi na ukomo wa aina moja ili kuzuia wengine kubadilisha katiba na kuwa marais wa maisha kama Robert Gabriel Mugabe wa Zimbabwe.
6. Viongozi wa Afrika wajitahidi katika matumizi ya rasilimali na kuhakikisha zinawanufaisha wananchi wake.
7. Pawepo na mahakama ya kisheria afrika badala ya kuwa na mahakama ya haki za binadamu ambayo haina meno kwa bara hilo la Afrika.
8. Wananchi waamke kupinga tawala za kidikteta na kufuatwa kwa utawala wa kisheria badala ya kuknyaga katiba na kuichezea kwa namna wanavyotaka.
Hata hivyo unatakiwa uzalendo wa hali ya juu kwa wananchi na viongozi wao ili kuhakikisha nchi zao zinaendelea kudumisha amani na utulivu na kuhakikisha kwamba nchi hizo zinatawalika.
By
MRUTU, ELIAS MARTIN.
0787032717
0715032717
0622032717
mrutuelias@gmail.com
mrutuelias@ymail.com
mrutu.elias@mnma.ac.tz

Related Surnames:
MRUTU

No comments yet.